Dawa Mkononi inalenga kutumia uvumbuzi kuboresha mnyororo wa usambazaji. Shughuli za Dawa Mkononi zinalenga hasa maduka ya dawa, vituo vya afya, na wateja wengine waliosajiliwa wa B2B. Kwa mbinu zake zinazotegemea data, tuna dhamira ya kuboresha upatikanaji wa usambazaji wa dawa na kuzifanya dawa zipatikane kwa urahisi zaidi kwenye vituo vya afya.
Dawa Mkononi ni bidhaa ya DMRX Inc., kampuni yenye makao yake Marekani. DMRX Inc. ni kampuni mama ya DMRX Company Limited, kampuni iliyosajiliwa Tanzania.
Kuongoza uvumbuzi wa dawa barani Afrika, na kufanya dawa bora zipatikane kwa wote.
Kuboresha upatikanaji na uwepo wa dawa katika jamii za Afrika.